Spotlighting Pan-African Poetry

Biography

Lolani Kalu

Featured Poem:

Kumebe Nimetekwa Nyara

Enlarge poem

Yalinifika ya mwaka, kule mbali kiungani, gari liliharibika, nikitokea kazini,
usiku ulipofika, nikapata mhisani, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..

Kwake nikapumzika, kajua na msalani, kinywaji niliposhika, kumbe kina kungu ndani,
pindi nikazuzulika, nikajilaza kitini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..

Chakula alichopika, kikawa ni biriani, nyute zikanidondoka, kingali huko jikoni,
mezani akikiweka, hana nguo maungoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..

Chakula hakikulika, nikauliza kunani akasema anitaka, hajui ninangojani,
Huku akichekacheka, kanisukuma kochini, kumbe ninatekwa nyara, na shangingi mswahili..

Ndipo aliponishika, na kunibusu shavuni, akanipiga mweleka, na kuniangusha chini,
nikawa nababaika, nalazimishwa kuzini, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..

Akili akaniteka, kanifanya hayawani, japo nilishawishika, sikuipata makini,
majuto yalinifika, na wasiwasi moyoni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..

Ukimwi ukinishika, atakuwa lawamani, atajibu mashtaka, kunitia taabani,
kwa kweli alinibaka, elewa wangu mwandani, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..

Usinione kuchoka, sinazo nguvu mwilini, nililala na wahaka, nililala ugenini,
nilipata hekaheka, lisilo kamwe kanuni, kumbe nimetekwa nyara, na shangingi mswahili..

Najua umeshtuka, na wala huniamini, lakini yakimwagika, ayazoaye ni nani ?
japo unipe talaka, ukweli nimebaini, kwamba nilitekwa nyara, na shangingi mswahili..

Nilifanya kutoroka, kupitia dirishani, akashindwa kunishika, niliporuka uwani,
ndio sasa nimefika, nimerejea nyumbani, jana nilitekwa nyara, na shangingi mswahili…

Translation

This is a melancholic and horror poem about the misfortune that grips an unsuspecting man, and there is no hope and no escape for him. This man’s day starts like any other ordinary day until his car breaks down, and although he receives help from a lovely lady, this lady ends up torturing and raping him. This is a brave poem, it address an issue that is not addressed often enough in society – the abuse of men. The poem is sang as per Swahili traditional poetry practices.

How does this featured poem make you feel?

 • Amazement (4)
 • Pride (2)
 • Optimism (1)
 • Anger (1)
 • Delight (1)
 • Inspiration (8)
 • Reflection (5)
 • Captivation (3)
 • Peace (3)
 • Amusement (6)
 • Sorrow (4)
 • Vigour (0)
 • Hope (1)
 • Sadness (7)
 • Fear (2)
 • Jubilation (1)

Comments

 1. Lolani kalu amechukua hatua isiyokuwa ndogo kujaribu kuangazia suala hili la ubakaji wa wanaume, tangu hapo la wanawake bado haliagaziwi ipasavyo , kwa wanaume ndo hakusemeki ! Hongera

  iffat

Your email address will not be published.

Biography

Lolani Kalu is a veteran Kenyan journalists, multi-linguist, musician, actor and comedian and Swahili poet. As a Journalist he has had a rare opportunity of interacting with Kenya’s diverse and rich arts and culture.

Lolani is the founder of Safari47.org, which was established as a way to identify, nurture and develop raw talent identified in 47 counties of Kenya.